Harusi

Kadi za harusi zinazofika WhatsApp — kuanzia michango hadi mlangoni

Harusi ina hatua nyingi: kamati, michango, kadi, ibada, tafrija na foleni mlangoni. InvitePro inaweka yote sehemu moja ili kamati ifanye kazi pamoja na wageni wapate kila kitu kwenye simu zao.

Mfano wa kadi ya harusi iliyochorwa na mfumo wetu wa kadi. Kadi yako itakuwa na jina la kila mgeni, idadi ya watu na QR yake.
Mfano wa kadi ya harusi iliyochorwa na mfumo wetu wa kadi. Kadi yako itakuwa na jina la kila mgeni, idadi ya watu na QR yake.

Kinachochosha kwenye maandalizi ya harusi

  • Kadi za karatasi

    Kuchapisha, kuandika majina kwa mkono na kuzunguka kugawa kadi — kisha kadi zinapotea au zinafika kwa kuchelewa.

  • Vikao vya michango

    Nani aliahidi kiasi gani, nani ameshalipa, nani bado — kwenye daftari au kwenye kundi la WhatsApp lisilo na mpangilio.

  • Foleni getini

    Kadi zinazokopiwa au kutumika mara mbili, na walinzi wanaohangaika kuhakiki majina kwenye orodha ya karatasi.

  • Hujui nani anakuja

    Idadi ya viti na chakula inakisiwa kwa sababu wageni hawajibu kama watakuja.

Jinsi InvitePro inavyosaidia harusi yako

  • Ibada na tafrija kwenye mwaliko mmoja

    Weka ukumbi, saa na ramani ya ibada pamoja na ya tafrija (reception). Mgeni anaona zote mbili kwenye ukurasa wake na anaweza kuziongeza kwenye kalenda.

  • Kadi SINGLE, DOUBLE au ya familia

    Kila kadi inaonyesha jina la mgeni, idadi ya watu inaowaruhusu, meza na QR code yake binafsi. Unaweza kuongeza cheo (Mhe., Dkt., Mch.) mbele ya jina.

  • Michango ya kamati

    Orodha ya wachangiaji, ahadi na malipo (M-Pesa, benki, taslimu). Kila mchangiaji ana ukurasa wake wa salio na jinsi ya kulipa, na anaweza kuripoti malipo — mweka hazina anathibitisha.

  • Kamati inashirikiana

    Alika wanakamati, mweka hazina na walinzi wa mlango kwa barua pepe, kila mmoja na nafasi yake, na ruhusa ya harusi hii tu.

  • Ukaguzi wa QR mlangoni

    Walinzi wanachanganua kadi kwa kamera ya simu. Mtandaoni, ukaguzi hulinda idadi ya watu wanaoruhusiwa kwa kadi. Bila intaneti, wahudumu huratibu milango; ukaguzi huhakikiwa mtandao ukirudi.

  • Asante baada ya harusi

    Tuma kadi ya shukrani kwa waliohudhuria — bure.

  • Ratiba na ukurasa wa tukio

    Wageni wanaona ratiba ya siku kwenye kiungo chao, na wanaweza kutuma mwakilishi, kutuma salamu au kuwasiliana na kamati. Ukipenda, fungua ukurasa wa tukio wenye mandhari, picha zenu, hadithi yenu na muziki.

Maswali

Tunaweza kuweka ibada na tafrija sehemu tofauti?

Ndiyo. Tukio lina ukumbi mkuu na sehemu ya tafrija (ukumbi, anwani, ramani na saa). Wageni wanaona zote mbili kwenye ukurasa wao wa mwaliko.

Kadi ya DOUBLE inafanyaje kazi mlangoni?

Kadi ya DOUBLE inaruhusu watu wawili. Mlinzi anaweza kuwaingiza wote kwa pamoja au mmoja mmoja; mfumo hauruhusu kuzidi idadi hiyo hata simu mbili zikichanganua kadi moja.

Wachangiaji wanalipa kupitia InvitePro?

Hapana. Michango inalipwa moja kwa moja kwenye Lipa namba au akaunti ya kamati. InvitePro inahifadhi ahadi na malipo, na mchangiaji anaweza kuripoti malipo yake ili mweka hazina ayathibitishe.

Tunaweza kutumia kadi iliyochorwa na mbunifu wetu?

Ndiyo, bure: pakia picha ya kadi kisha weka jina la mgeni na QR code juu yake.

Anza maandalizi ya harusi yako leo

Fungua akaunti bure, tengeneza harusi yako na jaribu kutuma kwa wageni wachache kwanza.