Kwa mawakala na wachapishaji

Uza kadi za mwaliko za kidijitali kwa wateja wako

Wateja wako wanapata kadi binafsi kwa kila mgeni kwa WhatsApp au SMS, majibu ya mwaliko na mapokezi ya QR mlangoni. Wewe unaendesha matukio yao yote kwenye akaunti moja ya InvitePro.

Ni kwa ajili ya nani

Yeyote ambaye wateja tayari wanamfuata kwa ajili ya harusi, send-off au kitchen party.

  • Maduka ya uchapishaji na stationery

    Tayari unauza kadi za karatasi. Ongeza kadi ya kidijitali yenye jina la kila mgeni.

  • Wabunifu wa kadi

    Buni kadi mara moja kwenye kibunifu cha kadi. Majina, namba na QR zinajazwa kwa kila mgeni.

  • Wapangaji wa matukio

    Endesha matukio ya wateja wako wote kwenye akaunti moja, kila tukio na orodha ya kazi na vikao vya kamati.

  • MC na wapambaji

    Ongeza mialiko na mapokezi mlangoni kwenye huduma unayowapa wateja wako tayari.

Unachopata wewe na wateja wako

Kila huduma ni bure. Unalipia jumbe za SMS na WhatsApp tu, kwa kila mgeni, kwa kila tukio.

  • Akaunti moja kwa wateja wote

    Unda tukio kwa kila mteja. Kila kamati inaona tukio lake tu, na unaweza kumpa mteja kiungo cha kuangalia tu.

  • Kadi kwa WhatsApp na SMS

    Kila mgeni anapata kadi na kiungo chake. Majibu yanarudi kwenye orodha ya wageni yenyewe.

  • Mapokezi ya QR mlangoni

    Wahudumu wanaskani kila kadi kwa simu. Unaona nani amefika papo hapo.

  • Michango na bajeti vimo

    Michango, malipo, vikao vya kamati na bajeti ya tukio ni bure kwa kila tukio.

Malipo yanavyokwenda

Unamtoza mteja wako bei unayotaka. Unailipa InvitePro jumbe zinazotumwa na kila tukio tu, kwa bei zilizo kwenye ukurasa wa bei. Tuulize kuhusu bei kwa mawakala wenye matukio mengi.

Jinsi ya kuanza

Hatua nne kutoka mazungumzo ya kwanza hadi tukio la kwanza.

  1. 1

    Ongea nasi

    Tueleze kuhusu biashara yako na matukio mangapi unayafanya kwa mwezi.

  2. 2

    Fungua akaunti ya mratibu

    Workspace moja kwa biashara yako. Ongeza timu yako na wateja wako.

  3. 3

    Andaa tukio la kila mteja

    Buni kadi, weka orodha ya wageni na chagua SMS, WhatsApp au vyote.

  4. 4

    Tuma, kisha pokea wageni siku ya tukio

    Nunua kifurushi cha jumbe cha tukio hilo, tuma mialiko na skani kadi mlangoni.