Kuposa na uchumba
Kuposa kwa mpangilio — kuanzia mwaliko hadi ratiba ya siku
Kuposa ni hatua ya kwanza ya safari ya ndoa: familia mbili zinakutana, wazee wanazungumza na ndugu wanashuhudia. InvitePro inawasaidia kuwaalika watu sahihi, kuwapa ratiba ya siku na kujua nani anakuja.
Kinachochanganya kwenye maandalizi ya kuposa
Ndugu wa pande mbili
Familia ya bwana na ya bibi zina orodha zao; ni rahisi mtu kusahaulika au kualikwa mara mbili.
Ratiba isiyojulikana
Wageni hawajui saa ya kuwasili, lini wazee wanaanza mazungumzo na lini sherehe inaanza.
Michango ya familia
Ndugu wanachangia maandalizi, na ni vigumu kujua nani ameshatoa na nani bado.
InvitePro kwa kuposa
Ratiba ya siku
Weka ratiba: kuwasili, utambulisho, mazungumzo ya wazee, chakula na burudani. Kila mgeni anaiona kwenye ukurasa wake kwa kitufe cha “Angalia ratiba”.
Kadi binafsi kwa kila familia
Kadi SINGLE, DOUBLE au ya familia yenye jina la mgeni, idadi ya watu na QR yake — kwa WhatsApp au SMS.
Majibu, mwakilishi na maswali
Wageni wanajibu “Nitakuwepo” au “Sitakuwepo”. Asiyeweza kufika anaweza kutuma mwakilishi kwa jina na namba ya simu, na yeyote anaweza kuwasiliana na kamati.
Michango ya maandalizi
Fuatilia ahadi na malipo ya ndugu, bure. Ukipenda, weka viwango vya mchango vya kupendekeza.
Ukurasa wa tukio
Fungua ukurasa wa tukio wenye mandhari, picha zenu, hadithi yenu na muziki unaocheza pale tu mgeni anapobonyeza.
Maswali
Tunaweza kuweka ratiba ya siku?
Ndiyo. Ongeza vipengele vya ratiba (saa, kipengele, maelezo na mahali). Wageni wanaiona kwenye ukurasa wao binafsi, na kwenye ukurasa wa tukio ukiuwasha.
Mgeni asipoweza kufika?
Anabonyeza “Sitakuwepo”, au “Tuma mwakilishi” na kuandika jina na namba ya simu ya atakayemwakilisha. Kamati inaona majibu yote kwenye orodha ya wageni.
Kadi ikimfikia mtu asiyehusika?
Anabonyeza “Sio muhusika”, na kamati inaona hilo kwenye orodha ya wageni ili irekebishe namba au jina.
Anza maandalizi ya kuposa leo
Fungua akaunti bure, tengeneza tukio na tuma mialiko ya kwanza kwa ndugu wachache.
Matukio mengine